uwakiki orphanage center

Deutsch | English | Swahili

Chama

Shule ya Vichekechea Kitahya

Chekechea ya Kitahya ni tofati kabisa kulinganisha na chekechea ya Ujerumani. Viambaza vya chekechea hiyo vimejengwa kwa kukandikwa kwa udongo na miti. Ndani hamna chochote, kama vile meza, viti n.k. Watoto kuwa wanakaa chini, hawana vitu vya kuchezea wala vifaa vya kuwafundisha. Chekechea ina vyumba viwili ambavyo vinatosha kwa watoto 25, wakati watoto waliopo ni 75, kwa hivyo inahitajika madarasa mengine zaidi. Mara nyingi inabidi watoto wafundishwa nje.

Watoto hugawiwa katika vikundi vitatu hutokana na uwezo wao wa ufahamu. Wanafundisha na walimu wawili masomo yafuatayo: hisabati, kusoma na kuandika, kiingereza, kilimo, afya na michezo. Shule huanza baada ya saa mbili.

Watotohufundishwa kwa njia ya mhadhara, maana yake mwalimu huongea muda mwingi na watoto hisikiliza, mwalimu huuliza maswala na watoto hujibu. Jinsi hiyo kufundisha ni vigumu sana kwa watoto ambao umri wao kuanzia miaka mitatu mpaka sita, kwa sababu watoto wadogo hawawezi kusikiliza muda mrefu sana pamoja na hali ya hewa joto huwachosha watoto haraka.

Mara nyingi watoto hwana vifaa vya kusoma, kwa sababu wazee (mara nyingi si wazazi wao bali ni walezi wao) hawana pesa zu kutosha. Kikundi cha UWAKIKI wakiwa na uwezo wanasaidia kwa kuwapo vifaa vya wanatumia yabao kwa kuandika. Kwa hazi ya hisabati wanatumia vifuniko vya soda na vijiti.

Pia kikundi hiki cha wanawake kiliwajengea baadhi ya watoto mahala pa kuishi familia zile zisizo ua uwezo. Mwaka 2004 watoto yatima kiasi cha 70 walisaidiwa.