Maana ya UWAKIKI ni Umoja wa wanawake wa kijiji cha Kitahya. Kitahya ni kijiji kidogo kilichoko kaskasini-magharibi ya Tanzania, mkoa wa Kagera. Mkoa huu wanaishi watu wa kabila ya Kihaya. Wahaya ni watu wabarimu sana. Watu hawa, wengi wao ni wakulima. Zao lao la biashara ni kwa mfano kahawa na mazao yao ya chakula ni ndizi, karanga, maharagwe, viazi vitamu…
Kuanguka kwa bei ya kahawa katika soko la dunia pamoja na kila vya Tanzania na Uganda imeathiri uchumi wa Tanzania kwa jumla. Kutokana na kila vya wenyewe ka wenyewe katika nji za jirani, kama vile Uganda na Rwanda (na Kongo) n.k. Na kutokana na Hali mbaya ya hewa pamoja na ukame imesabalisha kipato cha watu kughuka.
Muundo wa chama cha UWAKIKI
Chama cha UWAKIKI kimeanzishwa na akina mama katika mwaka 1986. Kutokana na hali mbaya ya maisha akina mama hawa waliamua kuanzisha chama hichi. UWAKIKI ni chama kina chojitegemea (NGO). Hadi sasa kuna wanachama 17 wanaojitolea. Mbali ya kushiriki kwenye UWAKIKI akina mama wana familia zao na kazi zao za binafsi. Wamejipa wajukumu kuwalea na kuwafundisha watoto yatima.
Hali ya kiafya mbaya sana katika mkoa wa Kagera.Takribau asilimia 40 ya wakaazi wa Kagera wana UKIMWI, ambacho ni kima kikubwa katika Tanzania nzima. Watu wengi hawana uweo kulipa matibabu. Zamani watu walipata matibatu bure katika Zahanati za Kiserikali. Kuanzia mwaka 1996 zahanati hizo zimekuwa za kibinafsi, ina maana matibabu hayakuwa bure tena.
Ukosefu wa chakula bora na maji safi husababisha maradhi mengi kama vile kipindupindu, utapia mlo, n.k. Pamoja na haya wakaazi huwa wanashamuliwa na Malaria na maradhi ya kupooza.