Mwaka 2001 watoto yatima 75 (umri wao kuanzia miaka mitatu mpaka sita) walisaidiwa na UWAKIKI. Watoto walichukuliwa na familia nyingine ambao waliwalea katika chekechea walifundishwa bila kulipa ada yoyote.
Mpango wa kuingia katika chekechea ni njia ya kuwatayarisha watoto kuingia katika shule ya msingi.
Pamoja na vifaa vya shule, watoto hupata chakula na madawa. Baada ya kumaliza chekechea watoto wanapatiwa sare za shule, ambayo ni kitu cha lazima katika shule za Tanzania.
Maeneo ya kufanya kazi
- Huduma bure za watoto
- Kufundisha watoto wa chekechea
- Kuhitathi mazingiri
- Matumizi bora ya mashamba katika kupanda miti na ukulima wa migomba na mimea mingine
- Kupanda migomba kwa eneo la ekari 200
- Mradi wa kilimo cha nafaka na migomba ili kupata chakula cha watoto
- Mifugo ya mbuzi na kuku
- Kusuka na kazi mbalimbali za mikono
- Huduma za madawa, vyakula, kuni, maji na nguo kwa wazee, wagonjwa na vizuka
- Kazi ya mikono, ufumaji, ususi na mapambo