Mustakbali wa UWAKIKI
Tukizungumza kuhusu mustakbali wa UWAKIKI kuna fikra nyingi na mipango mingi. Lengo hasa ni kuwasaidia watoto wa yatima wengi zaidi, ambao wana umri wa miaka mitatu mpaka saba, pamoja na kuongeza elimu katika tani mbalimbali, kama vile kazi zu ufundi. Imepangwa kuanzisha „Orphanage Nursery Centre (kituo cha watoto yatima)“ ili kukamilisha mipango hiyo.
Katika kitu hicho kutakuwa na:
- Chekechea kwa watoto yatima na shule ya msingi kwa watoto wakubwa
- Kuwafundisha takriban 120 watoto bila malipo
- Madarasa mbalimbali, maifisi, vyumba kwa kufanya semina na mikutano na karakana
- Madawa na huduma za kiafya kwa watoto
- Vyoo na zahanati
- Baadaye kuna mpango wa kujenga kitu cha malezi kwa siku nzima
Ardhi kwa ajili kujenga kitua hichi kimeshpatikana kwa gharam ya 3.000.000 Tsh. Ingehitajika zipatikana takriban 160.000.000 Tsh ili kukamilisha ujenzi wote. UWAKIKI wana uwezo kugharimia asilimia 3 tu ya kiasi hicho kilichotajwa. Wakaazi wa kijiji cha Kitahya wan nia kubwa kusaisia, lakini hata siku moja hawatoweza kupata pesa zote zinazohitajika. Ili hatimaye kufanyakisha mradi huu kunahitajika msaada kutoka kwa wakaazi wa kijiji, wanachama wa UWAKIKI, masaada kutoka wilayani pamoja na wafadhili wengine.
Ingawa pesa zu kujenga kituo chichi hazijapatikana, malengo yako dhahiri, kama vile.
Matatizo
- Kuhakikisha elimu bora ipatikane kwa wanafunzi na walimu (elimu yuu zaidi)
- Watoto wengi zaidi wajisajili katika chekechea
- Kuwasaidia familia za watoto yatima, ambao wenyewe wana shughuli nyingi za lazima za kimaisha
- Mradi huu uwe ni mfano mzuri kwa wanakijiji ili kuwahanasisha na wao